Advertisement
KUOGELEA

Tanzanite yatamba kutetea ubingwa 8 African Aquatics

Timu hiyo ya Taifa ya Kuogelea ya Tanzania, itashiriki michuano hiyo ikiwa na waogeleaji 30
Advertisement

Timu ya Taifa ya Tanzania ya mchezo kuogelea 'Tanzanite', imeondoka kwenda Rwanda kwa ajili ya mashindano ya 8 African Aquatics, Kanda ya Tatu ambayo yanatarajia kuanza Novemba 23-25.

Advertisement

Msafara wa kikosi hicho umeondoka ukiwa na waogeleaji 30, makocha 3 pamoja na viongozi 6.

Akizungumza na Pulsesports kuhusu mashindano hayo, Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), Inviolata Itatiro, amesema lengo la Tanzania kwenye michuano hiyo ni kutetea ubingwa wao ambao waliutwaa Novemba, mwaka jana.

Amesema wamefanya maandalizi mazuri ambayo yanawapa matumaini ya kufanya vizuri na kupeperusha vyema Bendera ya Taifa.

"Sisi kama viongozi tumefanya kazi nzuri kwa upande wetu katika kukijenga kikosi na tunaamini kuwa wana uwezo wa kufanya vizuri na kuiheshimisha nchi," amesema Itatiro.

Advertisement

Tanzania inkwenda katika michuano hiyo wakiwa kama mabingwa watetezi na wana kazi ya kulitetea taji hilo mbele ya mataifa 11 ambayo nayo yatashiriki.

Makocha watakaokuwa na jukumu la kuwaongoza waogeleaji hao ni Alexander Mwaipasi, Michael Livingstone na Zubery Yusuph.

Advertisement
Loading discussion…

Signing in with Google...