Advertisement
KANDANDA

Taifa Stars yaichapa Niger kufuzu Kombe la Dunia 2026

Mchezo huo ni wa kwanza kwa timu hizo kwenye Kundi E ambapo wenyeji Niger waliupeleka mchezo huo nchini Morocco
Advertisement

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', imeanza vyema kampeni ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Niger.

Advertisement

Mchezo huo ni wa kwanza kwa timu zote kwenye Kundi E ambapo wenyeji Niger waliupeleka mchezo huo nchini Morocco kutokana na nchini kwao kuwa na machafuko ya kisiasa.

Bao la ushindi katika mchezo huo lilifungwa kipindi cha pili dakika ya 56 na Charles M'mbobwa ambaye anacheza soka la kulipwa katika Klabu ya Macarthur ya nchini Australia na alikuwa akicheza mechi yake ya kwanza akiwa na Stars.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na mashabiki wachache, Stars ingeweza kufunga mabao zaidi kupitia kwa nahodha, Mbwana Samatta na Hajji Mnoga lakiki walikosa umakini kukwamisha mpira wavuni.

Dakika ya 73, Mnoga ambaye anacheza soka la kulipwa nchini Uingereza katika Klabu ya Aldershot United alikosa bao la wazi ambalo lingeweza kufanya ushindi kubwa mnono zaidi.

Advertisement

Kikosi cha Stars kinatarajia kurudi nchini kesho kwa kutumia ndege maalumu ambayo ilitolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na watakuja kujiandaa na mechi dhidi ya Morocco ambayo itachezwa Novemba 21 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Katika msimamo wa Kundi E, Stars sasa wana alama tatu sawa na Zambia ambao nao walishinda dhidi ya Congo Brazzaville.

Advertisement
Loading discussion…

Signing in with Google...