Advertisement
KANDANDA

Simba SC yawasimamisha Chama, Kapama kwa utovu wa nidhamu

Nyota hao sasa watapelekwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya klabu hiyo kwa hatua zaidi
Advertisement

Klabu ya Simba, imewasimamisha wachezaji wake, Clatous Chama na Nassoro Kapama kwa utovu wa nidhamu kwa muda usiojulikana.

Advertisement

Chama katika siku za hivi karibuni amekuwa akihusishwa kucheza chini ya kiwango huku akidaiwa kuihujumu timu baada ya kufungwa mabao 5-1 na Yanga SC Novemba 5.

Kapama bado anajitafuta kwani tangu kuanza msimu huu hajapata nafasi ya kucheza ndani ya timu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo, wachezaji hao baada ya kusimamishwa sasa watapelekwa mbele ya Kamati ya Nidhamu kwa hatua zaidi za kinidhamu.

"Uongozi wa Klabu ya Simba unapenda kuwakumbusha watumishi wake kuzingatia misingi ya maadili na nidhamu," imesomeka taarifa hiyo na kuendelea.

Advertisement

"Klabu haitosika kumchukulia hatua yeyote atakayethibitika kwenda kinyume na utaratibu huo."

Hata hivyo, klabu hiyo haikuweka wazi ni utovu gani wa nidhamu wachezaji hao wamefanya hadi kufikia hatua hiyo.

Taarifa zaidi zinadai, nyota hao wamechukuliwa hatua hiyo baada ya kujibizana na mashabiki na wanachama wao katika mitandao ya kijamii.

Simba kwa sasa wanajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi Mashujaa FC, mchezo utakaopigwa Jumamosi katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Advertisement
Loading discussion…

Signing in with Google...