Advertisement
KANDANDA

Azam yasajili nyota mwingine kutoka Colombia

Mchezaji mpya wa Azam FC, Yeison Fuantes, akitambulishwa kwa waandishi wa habari
Huyo ni Mchezaji wa tatu mpya kusajiliwa na timu hiyo katika usajili wa dirisha dogo unaoendelea
Advertisement

Klabu ya Azam FC, imetangaza kukamilisha usajili wa beki wa kati raia wa Colombia, Yeison Fuentes.

Advertisement

Mchezaji huyo, amesaini mkataba wa miaka mitatu akitokea Klabu ya Leones ya nchini kwao Colombia.

Huyo anakuwa ni mchezaji wa tatu wa kigeni kusajiliwa na Azam kwenye dirisha hili la usajili.

Tayari Azam walishatangaza kunasa saini ya mshambuliaji, Franklin Navarro kutoka Colombia pamoja na kipa raia wa Sudan, Mustapha Mohamed kutoka El-Marakh.

Kutokana na usajili huo, Azam pia wanatarajia kuacha baadhi ya wachezaji ili wabakiwe na wachezaji 12 wanaotakiwa kucheza mashindano ya Ligi Kuu Bara na yale ya kimataifa.

Advertisement

Hadi sasa mchezaji wa kigeni aliyetangazwa kuondoka ni Idris Mbombo pekee huku idadi ya wachezaji hao kwa Azam sasa ikiwa ni 14.

Advertisement
Loading discussion…

Signing in with Google...